This world cup is full of suprises
Yaani i wonder inakuwaje game zinakuwa tight hivi? halafu timu za africa tatizo lao ni discpline. Wangejirekebisha hapo mambo yangekuwa shwari.
Maombi yangu ni kwa timu ya africa kushinda world cup. i believe it is possible.
Naomba niwasilishe ombi moja, Kiukweli kabisa nimekuwa nikishabaikia timu ya yanga kwa takribani Miaka yote ambayo nimepata fahamu zangu. Lakini kwa kipindi chote hicho kusema kweli hizi timu zetu kongwe hakuna hata moja ambayo imefikia hatua ya mafanikio ambayo yanaonekana kwa macho kama hii timu ya AZAM. Kiukweli tangu imeanzishwa kama sikosei ilikiwa miaka mitatu nyuma Nimeifatilia sana na na nimegundua ndio timu inayopaswa ishangiliwe kwa nguvu zote. na naomba mungu asaidie iwe na mashabiki wa kuzidi timu zote hapa tanzania ili iwe funzo kwa Timu zote kubwa waweze kujirekebisha. Naomba pia nieleweshwe jinsi ya kujiunga na timu hii kama shabiki na mwanachama, ikiwezekana nipate na Kadi halali ya uanachama. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki AZAM FC.
Mwisho kabisa naomba mui-update hii website karibu kila siku.
mbona mmeifungia forum








aamsuni:
Mie sio mgeni katika safu zenu, leo nime kuja na mambo mawili matatu, ambayo kwa hakika yatatusaidia.
DUKUDUKU.
1. Profile za Player. Mara ya mwanzo nilikuwa na kuta kikosi kizima cha Azam A pamoja Azam B vilevile na benchi la ufundi kwa ujumla. Kila mchezaji kaelezewa ila aliyekuwa kaelezewa kiundani zaidi ni John Boko.
Cha ajabu sasa si wachezaji wote profile zao zinaonekana, na zile zinazonekana hazitoa maelezo ya kutosha juu ya mchezaji husika.
2. Rekodi za klabu. Tunafahamu kuwa Boko ndiye anayeshikilia rekodi ya kutikisa nyavu, ila haziko wazi hiyo rikodi katika website yetu pamoja na rikodi nyinginezo.
Ningependa kujua nani kafanya hiki katika klabu yetu kwa urahisi kabisa.
3. Makocha kuto tulia. Ni bado wachanga na tuna misimu mitatu katika ligi kuu, cha ajabu timu ishafundishwa na makocha wakigeni watatu. Nataraji huyu wasasa atakaa, na tumgee mda.
MAONI.
1. Suala la uwanachama tusilipe nafasi katika klabu yetu. Tubaki kuwa mashabiki na kama mtafikia uwamuzi wa wanachama, basi nguvu yao juu ya klabu izibitiwe.
Kwetu Tanzania soka la uwanachama bado, tuendelee kuwa mashabiki tu.
2. Timu yenu inakuwa na ni miongoni mwatimu ambazo zinaingiza mashabiki wengi viwanjani. Lazima muwe makini pale mtakapo weka majukwaa katika uwanja wetu wa chamazi kwa kuangalia wastani wa mashabiki wanaojitokeza kushuhudi mechi za azam.
PONGEZI.
1. Nalipongeza benchi la ufundi na kamati zima ya usajili kwa kufanya usajili mapema na ni tumai maandalizi ya msimu ujao yataanza mapema zaidi na huku kukiwa na mechi nyingi za kirafiki.
2. Jopo zima la habari, kwa kutujulisha kila linalo endelea ndani ya klabu.
Natumai msimu ujao tutaanza kuutumia uwanja wetu wa chamzi. Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki Azam fc.
www.aboodmsuni.blogspot.com