Ngasa akaribia kutua Simba SC... watoa ofa ya Milioni 25. Yanga waishia milioni 20

Hadi hivi sasa Ofa ya Simba ni shilingi Milioni 25 na Yanga ni Milioni 20. kutokana na hilo. Simba wapo kwenye nafasi kubwa ya kumnyakua Mrisho Ngasa. Kesho ni siku ya Mwisho. Ingawa tungependa kumuuza Mrisho Ngasa Yanga lakini tutampeleka kwa timu iliyotoa ofa nzuri zaidi

Lengo la Azam FC lilikuwa ni kumpeleka Mrisho kwenye timu ambayo atacheza kwa raha na amani, kutokana na yeye kuivaa na kuibusu Jezi ya Yanga siku ambayo Azam FC haikuwa na mchezo na Yanga... Azam FC inaamini kuwa Yanga ilikuwa Sehemu sahihi kwa Mrisho, lakini uongozi wa Yanga umeonekana kutokuwa na haja na Mrisho na ndiyo maana umeonekana kukataa kutoa ofa ya maana. Kutokana na sababu hizo Azam FC italazimika kumuuza Mrisho Ngasa Simba kwani hatuhitaji kuwa na mchezaji ambaye anafanya vitendo vya kuidharau brand ya Azam FC ambayo tunajaribu kuijenga.

Imetolewa na Utawala

Azam FC

Tags: 

Safi sana..

sie tunachoangalia ni faida timu yetu haiendeshwi kienyeji bana naona sasa na simba atachezea na kufanya kuwa moja ya wachezaji waliopata kuchezea timu kubwa kubwa hapa bongo bora tuchukue huo mkwanja tuendeleze uwanja wetu tu..

Forza Azam FC