Ushindi wa 3-0 dhidi ya Mgambo Shooting umeipeleka Azam FC CAF Confederations Cup ten kwa kuwa mshindi wa pili kwenye ligi kuu 2012/2013 na kupata nafasi nyingine ya kuiwakilisha Tanzania kwenye Mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Azam FC imepata ushindi huo wa nyumbani na kufikisha jumla ya pointi 51 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine yoyote iliyo nyuma yake, Azam FC ikitwaa nafasi ya pili, Yanga wiki tatu zilizopita ilitangazwa kuwa bingwa wa ligi hiyo huku Simba wakibaki katika nafasi ya tatu.
Read more...