C.E.O AZAM FC ALIPOHOJIWA NA BBC KUHUSU USAJILI WA WACHEZAJI AFRIKA

Category: 

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat', akiunga mkono kwa asilimia 100, kuwa kipindi cha uhamisho wa wachezaji kwa nchi za Afrika kinatakiwa kuendana ili kutoa fursa kwa timu kuziba mapengo au kuuza wachezaji kwenye klabu nyingine.

Popat ameunga mkono hoja hiyo, alipokuwa akifanya mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kwenye makala yao iliyokuwa ikiuliza kuwa: Je! Ni wakati wa kuungana kwa dirisha la uhamisho la wachezaji Afrika?

Makala hiyo pia imewahusisha waandishi wa habari mbalimbali barani Afrika, pamoja na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Afrika (CAF), Amaju Pinnick, ambaye amedokeza kuwa wataliangalia suala hilo.

CREDIT | BBC Sport Africa By Juliet Mafua

https://www.bbc.com/sport/africa/46978691

Back to Top